The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Wema Ahukumiwa Jela kwa Madawa ya Kulevya – Video

MREMBO na mwigizaji maarufu wa Bongo Movies, Wema Sepetu amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Tsh. Milioni 2 baada ya kukutwa na makosa mawili ya kutumia na kuhifadhi dawa za kulevya nyumbani kwake.

 

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Thomas Simba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Julai 20, 2018 ambaye amesema, Wema ametakiwa kulipa faini hiyo na kama akishindwa basi atapelekwa jela kutumikia adhabu hiyo.

 

Katika maamuzi mengine ya mahakama kuhusiana na kesi hiyo, wafanyakazi watatu wa ndani wa msanii huyo ambao waliokuwa wametajwa kwenye kesi hiyo wameachiwa huru na mahakama hiyo baada ya kutokutwa na hatia yoyote.

 

Wema ambaye ni Mshindi Namba Moja wa Taji la Misii Tanzania mwaka 2006, alikuwa akituhumiwa kwa makosa hayo mawili ya kutumia madawa ya kulevya aina ya bangi na kukutwa na madawa hayo nyumbani kwake.

 

WEMA TAYARI AMEWASILI, HUKUMU YAANZA KUSOMWA KISUTU

Comments are closed.