BREAKING NEWS: WEMA APATA DHAMANA, MAHAKAMA YAMUONYA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Jumatatu, Juni 24, 2019 imemwachia kwa dhamana Malkia wa Filamu Bongo, Wema Sepetu,  baada ya kukaa mahabusu ya Segerea kwa siku saba tangu Jumatatu iliyopita, Juni 17 kwa kukiuka masharti ya dhamana yake.

Aidha, mahakama hiyo imemuonya kwa kitendo chake cha kukiuka masharti ya dhamana na kumtaka kutorudia tena huku kesi yake ikitajwa kusikikizwa tena Julai 4, 2019.

Wema alionekana kuficha uso wake mara nyingi alipokuwa mahakamani hapo na baada ya kuachiwa kwa dhamana, aliwakwepa mapaparazi kwa kukimbia huku akipitia mlango wa nyuma wa mahakama hiyo ili asipigwe picha na wanahabari.

Mlimbwende huyo anakabiliwa na mashtaka ya kujipiga picha za ngono na mpenzi wake kisha kuzisambaza kupitia mitandao ya kijamii.

Matukio Katika Picha:


Loading...

Toa comment