The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Zitto Afunguka Makubaliano ya Serikali na Barrick – Video

0

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Zuberi Kabwe, amefungukia madai ya kuitwa kibaraka wa wazungu kwenye sakata la makinikia, ambapo amesema hawezi kuacha kuhoji kuhusu fidia iliyolipwa na Barrick Gold kuhusu sakata la makinikia, na kuendelea kusisitiza kwamba serikali inawadanganya wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Zitto amesema ni ukweli usiopingika kwamba wananchi wamedanganywa kwa sababu ripoti za Profesa Mruma na Profesa Ossoro, zilionesha kwamba kuna fidia ya zaidi ya trilioni 400 ambazo Acacia wanatakiwa kuilipa serikali, lakini matokeo yake, ni shilingi bilioni 700 tu zilizokubaliwa kulipwa.

Zitto alienda mbele na kueleza kwamba, maelezo kwamba Barrick Gold na serikali watagawana nusu kwa nusu mapato ya mauzo ya dhahabu, hayaeleweki kwa sababu Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Sheria na Katiba hajafafanua makubaliano hayo yanahusu nini zaidi.

NA DENIS MTIMA | GPL

Video Zitto Akifunguka

Leave A Reply