RAIS John Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuanzia leo Novemba 13, 2020. Prof. Kabudi alikuwa akishika wadhifa huo katika baraza la mawaziri lililopita.
Aidha, amemteua Dkt. Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango ambapo alikuwa akishika wadhifa huo katika baraza la mawaziri lililopita.



