The House of Favourite Newspapers

SHILOLE Afunguka! Mjengo Wake Mpya “Nina Tattoo 17” – Video

Msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole au ‘Shishi Baby’ baada ya kupata dili nono la kuwa balozi wa Taulo za kike aina ya HQ, ameweka wazi kuhusu mafanikio yake ambayo amekuwa akiyapata kila mwaka.

 

Akipiga stori na Global TV Online wakati wa kutangazwa rasmi kuwa balozi wa HQ, Shilole ambaye anafahamika kuwa mwanamke jasiri na mpambanaji, amesema siri ya kupewa shavu na makampuni mbalimbali, sababu yeye ni mkweli na muwazi hivyo makampuni mbalimbali humwamini na kumpa ubalozi.

 

Shilole ambaye pia ni balozi wa Shirika la Mawasiliano la Tanzania (TTCL) kupitia kampeni yake ya Rudi Nyumbani Kumenoga, ameweka bayana kuhusu mjengo wake mpya wa kisasa ambao tayari ameshahamia na anaishi na kuachana na maisha ya kupanga kama ilivyo kwa baadhi wasanii wenzake.

 

Mbali na muziki na ubalozi kwenye makampuni mbalimbali, Shilole pia amefahamika kuwa mjasiriamali wa upishi wa vyakula (mama ntilie) na kuvisambaza kwenye matamasha, mikutano na maofisi jambo ambalo linamuongezea kipato kikubwa.

VIDEO: MSIKIE SHILOLE AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.