The House of Favourite Newspapers

JPM: Wanajeshi Wamesomba Korosho, Waziri Upo Tu! – Video

RAIS  John Magufuli amewaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Lugha Bashungwa, Kamishna Mkuu wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Edwin Mhede na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, Charles Kichere. 

Vilevile, Magufuli amepokea gawio la Tsh. Bilioni 3 kutoka Kampuni ya mawasiliano ya Bhart Airtel ambayo inamilikiwa pia na serikali kama mwanahisa na Tsh bilioni 2, ambayo wamekabidhi Ikulu kama pongezi kutokana na mambo makubwa yanayofanywa na serikali.

 

“Kwa hawa walioapishwa, ninawapongeza lakini ninawapa pole, Watanzania wanataka ‘outcome’ (matokeo). Wanataka matokeo mazuri, kazi yangu ni kuteua ili kiu  yao iweze kuthaminika, kazi hizi ni za muda, aliyekuwa Waziri wa Viwanda haku-push kama nilivyotarajia.

 

“Nani aliwakataza mawaziri kuzunguka na kufanya mikutano na wafanyabiashara, na ndiyo maana wanasema hawamjui. Hata nikiuliza Manyanya watasema hawamjui, Watanzania sio wanafiki. Inaitwa Wizara ya Viwanda na Biashara, ni biashara gani iliyofanya.

 

“Watanzania wanataka kuona matokeo tutaelezana maneno mazuri lakini hakuna kitu, hayo maneno mazuri kaelezane na mke wako au mume wako. Wizara ya Kilimo imefanya kazi yake imenunua korosho na wanajeshi wamesomba, Wizara ya Biashara imefanya nini, ipo tu. Korosho zimekaa tumesubiri hadi mwezi wa tatu wanne, mpaka nchi za Benin, Nigeria wakazalisha, wizara husika ipo tu

 

“Natoa agizo kwa Waziri Bashungwa kufanya kazi kwa bidii kwa kutatua changamoto zilizopo zikiwemo za kuhakikisha viwanda vilivyobinafsishwa vinafanya kazi. Nakuamuru viwanda ambavyo vimefungwa sitaki uviorodheshe tu, nenda katafute wawekezaji pale uwaweke.

 

“Unaona kodi za ndani zinashuka na hakuna hatua yoyote inachukuliwa, unaona magari yanapakia bidhaa yakijifanya yanakwenda nchi jirani, yanakwenda hadi mpakani mtu anagonga mhuri kisha anarudi kushusha hapahapa nchini, unashindwa kuingilia hilo.

 

“Bila kodi hakuna nchi, hivyo nakuagiza Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Mhede ukafanye kazi hasa katika suala la Makamishna wa TRA waliopo mipakani ambao hawafanyi vizuri. Najua Njombe kuna changamoto nyingi hivyo nakuagiza Katibu Tawala Bw. Kichere ukafanye kazi, ukawashirikishe watu na kujenga mahusiano mazuri kati ya viongozi wa mkoani humo ili Njombe ibadilike.

 

TAZAMA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.