BREAKING: Rais Magufuli Kwenye Mkutano wa Hadhara Serengeti

Rais Dkt John Magufuli anaendelea na ziara yake ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo leo Septemba 06, 2018, amefanya mkutano wa hadhara wenye Uwanja wa Mwenge wilayani Butiama, mkoani Mara wakati akizindua barabara ya makutano ya Natta, Mugumu, Serengeti.

 

Rais Magufuli ametangaza rasmi kuwa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa Stiegler’s Gorge ukikamilika utaitwa ‘Nyerere Gorge’.

“Tukishafanikiwa huo mradi, hilo jina litapotea, tutaita Nyerere Gorge, utamuitaje Stiegler ambaye hujawahi hata kumuona… Nitalifuta hilo jina, kama nitafanya kosa, potelea mbali.

 

“Haiwezekani hapa Butiama alipolala Baba wa Taifa kukakosa maji, ninataka Waziri wa Maji, Makame Mbarawa ahakikishe anaanza haraka kutekeleza huo mradi mpya wa maji anaotaka kuuweka hapa.

 

“Wakuu wa wilaya, wa mikoa na maofisa ardhi mkae mtatue hii migogoro ya ardhi, msipoitatua maana yake mmeshindwa kuongoza, haiwezekani kukawa na migogoro mpaka watu kwenye msimu wa kilimo, kama mmeshindwa mniambie nilete wengine.

 

“Wananchi wanauhaba wa ardhi nyie viongozi mnataka kuweka wawekezaji wa sukari, wakati mwingine hivi viwanda vinavyowekwa mipakani muwe navyo makini, mtu anaweza kutumia njia hiyo kuingiza Sukari kutoka nje anakuja kuwauzia hapo.” amesema Magufuli.

 

Loading...

Toa comment