Breaking: Rais Samia Amteua Jaffar Haniu Achukua Nafasi ya Msigwa Ikulu -Video

RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Jaffar Mohamed Haniu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), akichukua nafasi ya Gerson Msigwa ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, kabla ya uteuzi huo, Haniu alikuwa mtendaji mkuu wa vyombo vya Africa Media Group LTD na uteuzi wake umeanza leo, Juni 9, 2021.Tecno


Toa comment