Kartra

Breaking: Rais Samia Apangua Mawaziri, Amteua Makamba, Mbarawa -Video

Rais Samia leo Septemba 12, 2021 amefanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za Uongozi kama ifatavyo:_

1. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua January Makamba kuwa Waziri wa Nishati akichukua nafasi ya Dkt. Merdard Kalemani ambaye uteuzi wake umetenguliwa

 

2. Rais Samia amemteua Dkt. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari anachukua nafasi ya Dkt. Faustine Ndugulile ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

 

3. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Stergomena Tax kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa anachukua nafasi ya Elias John Kwandikwa aliyefariki dunia mwezi Agosti 2021

 

4.Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Makame Mbarawa kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho uteuzi wake umetenguliwa

 


Toa comment