BREAKING: RAIS TSHISEKEDI AKAGUA BANDARI YA DSM – VIDEO

Rais wa Kongo, Felix Tshisekedi amepongeza ujenzi wa miundo mbinu inayoendelea nchini katika maeneo mbali mbali ikiwemo bandari ya Dar es Salaam na kusema kuwa itachochea ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi miongoni mwa wananchi.

Rais Tshisekedi ameyasema hayo leo wakati akitembelea miradi ya maendeleo nchini ikiwemo Mradi wa Reli iendayo kasi (SGR) na Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake ya siku mbili hapa nchini.

Aidha, katika hatua nyingine Rais Tshesekedi ameeleza adhma ya nchi yake kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuchochea maendeleo katika nchi hiyo inayoongoza kwa ukubwa barani Afrika.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amemweleza Rais Tshisekedi umuhimu wa Bandari ya Dar es Salaam kibiashara kutokana na mfumo wake kijiografia.

Ziara ya Rais Tshisekedi imehitimishwa kwa mkutano na Mwenyeji wake, Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo wamekubaliana kuimarisha mahusiano ya kiuchumi baina ya nchi hizi mbili.  

TAZAMA TUKIO HILO HAPA


Loading...

Toa comment