Breaking: Rais wa Chad Auawa na Waasi Baada ya Kushinda Uchaguzi

Rais wa Chad, Idriss Deby (68) amefariki dunia saa chache baada ya kutangazwa kushinda uchaguzi wa Urais kwa muhula wa sita.

 

Taarifa zilizotolewa na Jeshi la Chad na kutangazwa na redio ya taifa, Deby ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 30, amefariki baada ya kupata majeraha kwenye mapambano dhidi ya waasi wanaoshambuliana na majeshi ya serikali Kaskazini mwa Sahel, wakijaribu kuuteka mji mkuu, N’Djamena.

 

Taarifa zinaeleza kwamba baada ya matokeo kutangazwa na kuonesha kwamba Rais Deby ameshinda kwa asilimia 79.3 katika uchaguzi mkuu uliofanyika April 11, mwaka huu, aliamua kwenda kuungana na jeshi la nchi hiyo kupambana na waasi kaskazini mwa nchi hiyo ambako kwa bahati mbaya, alijeruhiwa na baadaye kupoteza maisha.

 

 Tecno


Toa comment