Breaking: Sabaya Ashtakiwa kwa Ujambazi – Video

Image

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ambaye alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, amesomewa mashtaka sita, ikiwemo uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, wizi wa simu na unyang’anyi wa kutumia silaha (ujambazi).

 

Sabaya ambaye amefikishwa mahakamani hapo leo mchana Ijumaa Juni 4, 2021 akiwa na watuhumiwa wenzake wanne, mbele ya mahakimu wawili na wamesomewa makosa hayo sita na kunyimwa dhamana hadi Juni 18 kesi yake itakapotajwa tena.Tecno


Toa comment