The House of Favourite Newspapers

BREAKING: SHAFFIH DAUDA AACHIWA KWA DHAMANA KISUTU

Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu imewapandisha kizimbani, Benedict Kadege na Shafii Dauda wakikabiliwa na shtaka la kutumia maudhui mtandaoni bila kuwa na kibali cha Mamlaka ya ya Mawasiliano TCRA.

Wakili wa serikali Mkuu, Tumaini Kweka akishirikiana na mawakili Mutalemwa Kishenyi na Mwanaamina Kombakono wamewasomea shtaka hilo washtakiwa hao mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina.
Akisoma shtaka hilo wakili Kombakono amedai kati ya Juni 14 hadi Septemba, mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa kutumia Online TV inayojulikana kwa jina la Dauda TV, na Blogu yenye jina la shaffihdauda.co.tz kinyume cha sheria walitoa maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali cha TCRA.
Baada ya kusomewa shtaka hilo moja washtakiwa hao walikana na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Jebra Kambole ameomba wateja wake wapewe dhamana kwa sababu shtaka linadhaminika.
Upande wa Jamhiri chini ya wakili Tumain umedai hawapingi kutoa dhamana ila kama mahakama itaridhia kutoa dhamana izingatie kifungu cha 148 (6)(7) cha sheria ya makosa ya jinai. Hakimu Mhina ametoa masharti kwa washtakiwa hao ambapo amemtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya kuwatambulisha na barua ambazo zinatambulika kisheria.
Na kila mdhamini ametakiwa kusaini bondi ya Shilingi milioni 15 na kutoruhusiwa kusafiri nje ya nchi bila kupata kibali cha mahakama huku wakitakiwa Oktoba 8, mwaka huu kuwasilisha mahakamani hati zao za kusafiria. Washtakiwa hao wamepata dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 8, mwaka huu kwa a jili ya kutajwa.

BREAKING: Soudy Brown, Maua Sama, Shaffih Watinga Kortini Kininja

Comments are closed.