The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Watu 49 Wauawa Katika Shambulio la Kigaidi New Zealand

WAZIRI Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern, amesema watu 49 wameuawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch huko New Zealand.

 

Waziri mkuu huyo amelitaja shambulio hilo kuwa lililotanda ‘kiza kikubwa’ siku ya leo nchini humo.

Wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa na Kamishna wa Polisi, Mike Bush, ameonya kwamba huenda washukiwa zaidi wapo.

Anayedaiwa kufanya shambulio hilo, Brenton Tarrant,  baada ya kujichukua kwa kamera mwenyewe.

 

Inaarifiwa kwamba washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali.

 

Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison, amesema miongoni mwa waliokamatwa ni raia wa Australia.

Amemtaja mshukiwa wa shambulio hilo kuwa “gaidi mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia”.

Wakati wa shambulio.

Walioshuhudia mkasa huo wameviambia vyombo vya habari kwamba walilazimika kutoroka kuokoa maisha yao na waliona watu walioanguka chini na wanaovuja damu nje ya Msikiti wa Al Noor.

 

Polisi inasisitiza kwamba hali bado haijaimarika na wamethibitisha pia kwamba “vilipuzi kadhaa vilivyofungwa kwenye gari vimeharibiwa.”

 

Maofisa wameshauri misikiti yote katika mji huo ifungwe mpaka ilani itakapotolea, wakieleza kwamba hili lilikuwa shambulio la vurugu ambalo halikutarajiwa.

 

Mohan Ibrahim, ambaye alikuwa katika eneo hilo la Msikiti wa Al Noor ameliambia Gazeti la Herald: “Awali tuliona ni hitilafu za umeme lakini mara tu, watu wote wakaanza kukimbia.

“Bado rafiki zangu wamo ndani. Nahofia usalama wa maisha ya rafiki zangu.”

Bado haijulikani wazi nini kilichofanyika ndani ya misikti hiyo ila imeripotiwa mshambuliaji alilenga sehemu ya maombi ya wanaume, na baadaye kuelekea katika sehemu ya wanawake.

 

Watu wamehamishwa pia kutoka msikiti wa pili katika kitongoji cha Linwood na kamishna wa polisi amesema:  “Watu kadhaa wameuawa” katika maeneo mawili.

Comments are closed.