Breaking: Soko la Kariakoo Laungua Moto


Breaking News: Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa, Soko Kuu la Kariakoo lililoko Ilala jijini Dar es salaam linawaka moto muda huu.

 

Kwa mujibu wa mmoja wa walinzi wa eneo hilo ambaye ameshuhudia tukio hilo amesema moto huo umeanza majira ya saa 2 usiku huku akieleza kuwa chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme iliyotokea katika moja ya duka lililopo katika jengo ambalo linateketea.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalaa, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto wote tayari wapo eneo la tukio.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalaa, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, Meya wa Ilala, Omary Kumbilamoto na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto wote tayari wapo eneo la tukio.

 

Kwa mujibu wa kamanda wa kikosi cha zimamoto ameeleza kuwa magari ya zimamoto yaliwahi kufika eneo la tukio na kupambana na moto huo lakini waliishiwa maji wakafuata maji mengine.

 

Amesema kuwa kuwa kwa awamu hii ya pili baada ya magari kurejea wana uhakika wataudhibiti moto huo kwani kuna magari sita ya zimamoto kitoka Wilaya ya Ilala, Temeke, Kinondoni, Uwanja wa Ndege na Bandarini ambayo yote yameuzingira moto huo.

 

Aidha, Kikosi cha Zimamoto kimetoa rai kwa wafanyabiashara wanaotaka kuingia ndani kutoa mali zao waache ili jeshi hilo liendelee na kazi yake ya kuzima moto.

Taarifa zaidi kukujia.

#globalhabariupdates

 


Toa comment