Breaking: Sokombi, Masele Watimka Chadema

#BREAKINGNEWS: Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Joyce Sokombi na Sussane Masele wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi mara baada ya kuhitimishwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Wabunge hao wameeleza sababu za kuhama kuwa  ni pamoja  na CHADEMA kutokuheshimu katiba yake ikiwa ni pamoja  na wabunge wanne wa chama hicho kufukuzwa uanachama bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.

“Wabunge wa viti maalum kila mwezi tunachangia chama Milioni 1.5, kila mmoja amechanga milioni 62, tuko wabunge 37 hivyo tumechangia jumla ya Bilioni 2.2. hatulalamiki kuchanga kwani ipo Kikatiba. Matumizi ya fedha hizi hayajawahi kuwekwa wazi na haturuhusiwi kuhoji popote

“Madaraka ndani ya CHADEMA yanahodhiwa na wachache wengi wao wakiwa wanaume na hivyo kuwepo mwanya wa unyanyasaji wa kijinsia na kingono” Wamesema Wabunge hao.

 

 

Masele na Sokombi ni miongoni mwa wabunge wa Chadema waliotakiwa na Kamati Kuu ya Chadema kujieleze juu ya uamuzi wao wa kukiuka makubaliano ya chama ya kukaa karantini kwa siku 14 huku wenzao wanne wakitimuliwa uanachama.

 


Toa comment