The House of Favourite Newspapers

Steve Amjibu Muna, ‘Usipomwamini Mungu Utamwamini Shetani’ – Video

Kufuatia mkutano alioufanya muigizaji Muna Love na waandishi wa habari hapo jana na katika maelezo yake akaanika sauti ya muigizaji mwenziye Steve Nyerere ambayo alimpigia simu muda mfupi baada ya mwanae kufariki dunia huko Kenya na kuzungumza nae baadhi ya mambo kuhusiana na kifo hicho cha mwanae.

 

Katika mazungumzo yake Muna, amekanusha baadhi ya taarifa ambazo zilitolewa na Steve Nyerere zikidai kuwa muigizaji huyo amekubali kushirikiana na Mumewe Peter Komu katika kumzika mtoto Patrick ambaye Muna amekanusha kuwa sio wa Peter bali ni wa Casto Dickson.

Sasa baada ya ubuyu huo kutua mezani kwa Steve Nyerere naye ameamua kuitisha mkutano na waandishi wa habari kupangua hoja zote zilizotolewa na Muna ambazo zinamuhusu yeye.

 

“Kwanza nimpe pole dada yangu Muna kwa kupita katika kipindi kigumu sana, kwa kuondokewa na mtoto. Tulikuwa tumejipanga kwenda kumuona, tukaambiwa kwa waliokoka huwa hawana 40, lakini kwa mzazi lazima kuwepo na 40. Mimi siyo mjinga wa kukurupuka tu kutangaza kuhusu msiba bila kuambiwa na wahusika wa msiba, sikukurupuka, mimi ni mtu mzima, nina familia na watoto, nilipewa maagizo hayo na Muna mwenyewe akiwa na ‘mumewe’ Joel Lwanga wakiwa Kenya, alinipigtia simu.

 

“Pale Leaders, mama mchungaji aliwambia Muna na Peter yaliyopita si ndwele mgange yajayo, yule mama anajua, inamana naye alidanganywa? Ningekuwa mchungaji nisingekuwa na imani na muumini wa namna hiyo, sifa ya aliyeokoka ni kusema ukweli. Familia nzima ya Muna kuanzia mama yake, ndugu na Mainda rafiki yake na kipenzi walikuwa Mwananyamala, lakini hili lililofanyika ni kufedhehesha akina mama.

 

“Nimemsikia akizungumza maneno mazito, eti nyumba anayoishi Peter haina hati, kama haina hati basi itakuwa ni ya serikali wakachukue nyumba yao. Anatukandamiza na kutoa voice, ametoa hisia zake kwa Watanzania, ametufundisha sisi vijana na wazee. Tukisema tufuatilie tutakuta mtoto uliyemsomesha hadi chuo kikuu ni wa mlinzi, mwanamke mwenye busara lazima awe na staha, ndoa siyo kitu cha mchezo jamani.

 

“Nimemsamehe Muna kwa sababu hajui kama anachokizungumza anakifahamu. Hili liwe funzo kwa dada zetu, mimi nimemsamehe hata nikikutana naye asiogope kunisalimia, Shilole naye amemsamehe, usipoimamini biblia utamwamini shetani,” amesema Steve.

 

Na Edwin Lindege | Global Publishers

 

MSIKIE STEVE NYERERE AKIFUNGUKA

 

Comments are closed.