The House of Favourite Newspapers

BREAKING: SUZAN KIWANGA ATIMULIWA BUNGENI HADI 2019

Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtoa nje ya bunge, Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema) na kumtaka kutohudhuria vikao vya bunge hadi Bunge la Bajeti mwakani baada ya kuingilia hoja Mbunge wa Tandahimba Katani Ahmed Katani aliyekuwa akikanusha kujiuzulu ubunge.

Ndugai amemtaka Kiwanga kutohudhuria kikao cha mkutano wa bunge uliyobaki ambao (utafanyika keho kabla ya bunge hilo kufungwa na Waziri Mkuu hadi mwakani 2019, huku akimtaka kutoshiriki mikutano ya kamati za bunge na michezo ya bunge.

Mapema leo taarifa za uzushi zilisambaa mitandaoni zikieleza kuwa, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Mtwara (CUF), Katani Ahmadi Katani, amejiuzulu Ubunge wa Tandahimba leo Alhamisi, Novemba 15, 2018 kutokana na mijadala iliyoko ndani ya chama hicho jambo ambalo amekanusha bungeni jioni hii.

Comments are closed.