BREAKING: UCHAGUZI WA YANGA WAHAIRISHWA – VIDEO


Kamati ya Uchaguzi ya TFF imesitisha uchaguzi wa Yanga uliokuwa ufanyike Jumapili ya tarehe 13, 2019, hadi itakapopokea oda ya Mahakama.

 

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ally Mchungahela amesema mchakato wa uchaguzi huo umesitishwa baada ya baadhi ya wanachama kufungua kesi katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Morogoro.

 

“Hatutaki kwenda kinyume na mahakama, tumeamua kusitisha mchakato huo hadi tutakapopata oda ya mahakama,” alifafanua Mchungahela.

Alisema mchakato wa nini kitaendelea kuhusu uchaguzi huo itajulikana Jumatatu: “Tunaomba wagombea wote wasitishe kampeni kuanzia sasa, “alisema.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment