The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Mbowe, Matiko Kurudishwa Gerezani, CHADEMA Watoa Tamko ZITO!

KUFUATIA Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwafutia dhamana Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kisha kupelekwa katika Mahabusu ya Gereza la Segerea leo hadi kesi yao itakapomalizika, uongozi wa chama hicho kupitia kwa katibu mkuu wake wametoa tamko.

 

“Dhamana huwa ni hukumu ya kwanza Mahakamani, dhamana ni hukumu ya kwanza Mahakamani, kufuta dhamana ni ngumu sana kuishawishi jamii kwa yale waliyofanya ni makubwa kiasi cha kustahili adhabu ya kufutiwa dhamana. Hii ni kumuadhibu mtu mara 2, akiwa nje, umesikiliza maelezo ya awali (P.H), anakuja unamfutia dhamana kwa kosa hilo hilo, anaadhibiwa sasa hivi ni mara ya 2, hatujui mara ya 3 atakuja kuadhibiwa nini.

 

“Katika kesi hii kulikuwa na Wadhamini wameweka bond zao pale, Je inakuwaje? kwanini na wao hawakuitwa kueleza, kwa sababu wadhamini wana mkataba na Mahakama kwa kuhakikisha huyu mtu anafika Mahakamani, mwenendo wa kesi hii inatia ukakasi katika utoaji haki.

 

Tumekuwa na wakati mgumu sana na Hakimu katika kesi hii, jinsi anavyotoa huduma, mpaka ikapelekea kutokuwa na imani naye, na kumuomba suala hili alikabidhi kwa watu wengine ambao wataweza kutoa haki inayoonekana,haki inatakiwa ionekane inatendeka.

 

“Leo tumeona muendelezo wa yale yale hata kama haki imetendeka lakini haki ambayo sisi tunaamini kabisa haijaonekana kutendeka mbele ya macho ya watu, Kwa msingi haki haijatendeka sababu hatujaona haki ikitendeka. Tumeamua kukata rufaa, tumeshawasilisha rufaa yetu Mahakama Kuu, katika rufaa yetu tumeeleza mashaka yetu juu ya mwenendo mzima wa hii kesi, tumeeleza ndani ya rufaa, tunaamini haki itandeka.

 

“Tunataka wanachama nchi nzima popote pale walipo, suala hili ni zito ni nyeti linahusu mustakabali wa Taifa letu, msisubiri kusimuliwa, njoo nwenyewe ujionee kinachoendelea Mahakamani,kwa sababu kumekuwa na upotoshaji mkubwa, utaambiwa vitu ambavyo havikutokea.

 

“Tunataka wanachama na wapenda haki wote Tanzania kuchukua hatua, tunaiomba Mahakama iangalie jinsi mwenendo wa kesi hii unavyoendeshwa na ijiridhishe kama kweli ndo namna ambavyo wao wangependa mashauri ya jinai yaendeshwe katika Taifa hili.

 

“Tunaomba wanachama na wapenda haki wote Tanzania mje msikilize wenyewe kesi hii Mahakamani, ili tujue nini kinaendelea na baada ya hapo tutajua ni hatua gani tutachukua sisi kama watetezi wa haki za watu wote katika Taifa hili, Asanteni.

 

Na hili liwe funzo kwa Wabunge, Madiwani, Kiongozi yeyote ndani ya Chama, mwanachama wa kawaida atakaebainika kukiuka Katiba, Kanuni na Taratibu za Chama, itategemea na kosa lakini onyo kali, adhabu zinazoendana na kosa atachukuliwa.

 

“Ndo kwanza kumepambazuka, anayeona ni jioni huyo ameshiba, lakini kwa sisi wenye njaa na kiu ya haki, ndio kwanza jua linachomoza Asanteni,” amesema  Dkt. Mashinji.

 

TAZAMA VIDEO HAPA AKIFUNGUKA

Comments are closed.