Breaking: Wagonjwa wa Corona Wafikia 25 Tanzania
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza kwa idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini imeongezeka na kufika 25. Taarifa ya Waziri wa wizara hiyo Ummy Mwalimu imeeleza kuwa mgonjwa aliyeongezeka ni mwanaume mkazi wa Dar es Salaam.


