The House of Favourite Newspapers

Breaking: Watu 11 Wakamatwa kwa Tuhuma za Kukutwa na Dawa za Kulevya Akiwemo Kocha wa Simba – Video

0

Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya miongoni mwao akiwa ni Kocha wa Makipa wa Simba Muharami Mohamed ‘Shilton’.

 

Hayo yameelezwa leo Novemba 15, 2022 na Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

 

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mamlaka hiyo imesema iliendesha Operesheni katika maeneo mbali mbali ya nchini na kukamata Jumla ya Kilo 34.89 za dawa za kulevya aina heroin pamoja na kukamata biscut 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa za kulevya aina ya Bangi kama moja ya Malighafi.

 

Mtuhumiwa mwingine miongoni mwa hao waliokamatwa ni Kambi Zubeir Seif ambaye ni Mfanyabishara na Mmiliki wa Kituo cha Michezo cha Cambiasso kilichopo Tuangoma, Kigamboni Dar es Salaam.

Leave A Reply