The House of Favourite Newspapers

Breaking: Watu 44 Wafariki, 37 Waokolewa Wakiwa Hoi Mwanza – Video


HABARI zisizothibitishwa zimeeleza kuwa watu kadhaa wamefariki baada ya kivuko cha  MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na Kisiwa cha Ukara  katika Ziwa Victoria (wilayani Ukerewe mkoani Mwanza) kuzama. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana, amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara na kwamba kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa 8:00 mchana kilipinduka.

Aidha, amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho na Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda, amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko ambapo  watatoa taarifa baadaye.

Wanajeshi na raia wamejitolea kutoa msaada wa uokoaji​ kwa miili ya marehemu na majeruhi wa ajali hiyo huku ikidaiwa kuwa kivuko kilikuwa kimebeba watu zaidi ya 400.
Updates: SAA 3:00 Usiku
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amesema idadi ya watu waliofariki kwa ajali hiyo imefikia 44 huku 37 wakiolewa lakini halo zao ni mbaya huenda vifo vikaongezeka.
Aidha, Mongela mesema Zoezi la uokoaji limesitishwa kwa muda hafi kesho asubuhi kutokana na giza kuingia.

BREAKING: Kilivyozama Kivuko cha MV NYERERE Leo

Hali ilivyo Usiku Huu Ziwa Victoria Miili Yaongezeka

Comments are closed.