The House of Favourite Newspapers

Lugola Amtaka OCS Chang’ombe Kuwaachia Huru Watuhumiwa – Video

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemtaka Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS), Chang’ombe, Temeke, jijini Dar es Salaam kuwaachilia huru mara moja watuhumiwa wote walioshikiliwa kituoni hapo bila hatia yoyote.

Lugola ametoa agizo hilo leo Jumanne, Novemba 20, 2018 alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo na kumtaka OCS huyo kupitia majalada yote ya watuhumiwa ili kubaini wenye makosa na wasiokuwa na makosa, waachiliwe ama kupewa dhamana kutokana na makosa yao kudhaminika.

 

Aidha, Lugola amesema ziara yake hiyo  ni mwendelezo wa ziara zake za kushtukiza katika vituo vya polisi, lengo likiwa ni kuimarisha utendaji kazi wa jeshi hilo kwa wananchi na kwamba ataendelea kushtukiza kwenye vituo vingine kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki za haki zao.

Katika hatua nyingine, Lugola amekiri kutambua kauli ya kwamba kuingia Polisi ni bure lakini kutoka ni pesa na kuamua kufanya ziara kama hiyo ili kushughulika na kauli kama hiyo ili wananchi wafurahie jeshi lao.

 

Kuhusu shamrashamra za Sikukuu ya Maulid, Lugola amewahikishia wananchi kuwa na amani na utulivu na kwamba hii ni fursa kwa jeshi la polisi kuthibitisha utendaji wake kwa wananchi kwa kulinda amani na utulivu uliopo.

Msikie Lugola Akifunguka

Comments are closed.