The House of Favourite Newspapers

Breaking: Rais Samia Atanga kifo cha Mzee Cleopa David Msuya – Video

Mzee Cleopa David Msuya, aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania na Waziri Mkuu enzi za uhai wake.

Rais Samia Suluhu Hassan amelitangazia taifa kifo cha Mzee Cleopa David Msuya, aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania na Waziri Mkuu, kilichotokea leo Mei 7, 2025 majira ya saa tatu asubuhi katika Hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam.

Rais Samia ametangaza siku saba za maombolezo.