Breaking: Yanga Yatangaza Kuachana na Feisal Salum Yamuuza Kwa Azam FC
Klabu ya Yanga imefikia makubaliano ya kuachana na nyota wake Feisal Salum ‘Fei Toto’ baada ya kukaa katika mgogoro wa muda mrefu.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwaomba Yanga kumaliza mgogoro na kiungo huyo Mzanzibari, ili mambo mengine yaendelea.
Fei aliingia kwenye mgogoro huo, baada ya kuvunja mkataba bila kuzingatia kanuni, hadi kesi kupelekwa kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) bado Yanga ikawa kwenye upande wa haki.