Kartra

Breaking: Yusuf Manji Arejea Tanzania

Taarifa zilizotufikia katika dawati letu la Habari ni kwamba mfanyabiashara maarufu nchini ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewasili nchini Tanzania leo Jumanne, Juni 1, 2021 jioni baada ya kukaa nje ya nchi kwa miaka kadhaa sasa.

 

Manji ambaye alijuwa akitajwa kuwa wakati wowote atarejea nchi amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo alihojiwa kwa muda kadhaa na maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuhusu uhalali wake wa kuingia nchini.

 

Imeelezwa kuwa baada ya kutoa maelezo yake, aliachiwa baada ya maofisa hao kujiridhisha kuwa Manji ni Mtanzania na anayo haki na uhalali wa kuingia nchini Tanzania.


Toa comment