The House of Favourite Newspapers

BREAKING: ZITTO AMKABIDHI KAZI MAALIM SEIF – VIDEO

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe,  amemkabidhi maalim Seif Hamad kadi namba moja ya chama hicho ambayo imeshalipiwa kwa kipindi cha miaka 10 kwa ajili ya kuanza rasmi kazi ya siasa ndani ya chama hicho.

 

“Mimi nina kadi namba nane… Kadi namba moja kuna mtu aliiwahi na kwa heshima kadi hii imekwenda kwa Maalim Seif,” amesema Zitto.

 

Shughuli ya kukabidhi kadi hizo imefanyika leo Machi 19, 2019, makao makuu ya chama hicho yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Viongozi wengine ambao wamekabidhiwa kazi ni Ismail Jussa, Mbalala Maharangande, Sheweji Mketo na mmoja wa wanasiasa machachari,  Juma Duni Haji, amekabidhiwa kadi namba kumi.

 

”Kadi maalumu zimekuwa nyingi kwelikweli maana tumepokea watu muhimu mpaka ilibidi tunyang’anyane lakini namba 1, 6, 10 na 17 zote zimekwenda kwa viongozi walioambatana na Maalim,” alisema Zitto.

 

”Naomba tusiingie kwenye mtego wa msajili, hivyo tutakwenda kusajili kadi zetu kwenye matawi yetu ili tusije kuulizwa kama makao makuu kuna tawi,” amesema Zitto Kabwe.

 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi, Maalim Seif, amesema yeye ni mara ya kwanza kukanyaga ofisi za ACT- Wazalendo lakini anajiona ni mwenyeji.

 

SHUHUDIA TUKIO HILO

Comments are closed.