The House of Favourite Newspapers

BREAKING: JPM AAGIZA KIVUKO KIPYA KIJENGWE HARAKA UKEREWE

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Kamwelwe kutangaza zabuni haraka kwa ajili ya kujenga kivuko kipya cha Ukara baada ya MV Nyerere kuzama.

 

Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kisiwani Ukerewe alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu shughuli ya uokoaji inavyoendelea na kusema kwamba hicho kipya kitakuwa na ukubwa mara mbili ya MV Nyerere kilichokuwa na tani 25 pekee na uwezo wa kubeba watu 101 kwa sababukivuko kipya kitakuwa na tani 50 na uwezo wa kubeba watu zaidi ya 200.

 

Majaliwa jambo hilo litasaidia kurudisha usafiri haraka katika eneo hilo la wakati MV Nyerere ikifanyiwa ukarabati baada ya kunyanyuliwa na Jeshi la Wananchi ambalo linakadiriwa kukiinua kivuko hicho kitaalam kwa siku mbili.

 

Aidha, Majaliwa amesema miili itakayoopolewa kuanzia leo itapelekwa katika Kituo cha Afya Busya na kuzikwa eneo maalum lililotengwa na serikali.

VIDEO: MSIKIE MAJALIWA AKIZUNGUMZA

Comments are closed.