BreakingNews: Mo Dewji Atekwa na Watu Wasiojulikana – Video

Mfanyabiashara maarufu nchini ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wakiwa na silaha za moto wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo Oktoba 11, 2018.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, inasemekana watu hao wamefyatua risasi hewani kuwatishia watu walikuwa karibu na eneo hilo kabla ya kuondoka naye.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo; “Tumepokea taarifa za kudaiwa kutekwa kwa mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji, kwa sasa bado ni taarifa tu, tayari tumeanza kuzifanyia kazi,” amesema RPC Muliro.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa amesema polisi wanafuatilia undani wa tukio hilo. Ametoa taarifa za awali kuwa waliohusika tukio hilo ni watu wawili ambao ni raia wa kigeni.

Tutaendelea kukupa taarifa zaidi.

Loading...

Toa comment