The House of Favourite Newspapers

BREKING NEWS: Al-Shabaab Washambulia Westlands Nairobi – Video

MAGAIDI sita wa Kundi la Al-Shabaab wamethibitisha kushambulia kwa mabomu na risasi eneo la 14 Riverside, Westlands karibu na Hoteli ya DusitD2 jijini Nairobi leo, Januari 15, 2018, saa 9:30, alasiri.

Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na Hospitali ya Aga Khan huku idadi kamili ya wanajeshi waliofariki ikiwa haikujulikana.

 

Msemaji wa kundi la Kigaidi la al-Shabab amepigia BBC simu na kudai kwamba kundi hilo limehusika katika operesheni ambayo bado inaendelea Nairobi na kwamba watatoa maelezo zaidi punde operesheni yao ikikamilika. “Watu wetu waliingia ndani na bado wako ndani ya majengo muhimu mtaa wa Westlands, Nairobi,” amesema kiongozi huyo.

Maofisa wenye utaalamu wa kutegua mabomu wamewasili katika eneo la tukio.Gazeti hilo pia linaripoti kuwa majeruhi wa mkasa huo wanakimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na Hospitali ya Aga Khan. Mpaka sasa Kikosi maalumu cha Recce Squad kimewasili eneo la tukio ili kuongeza nguvu ya uokozi wa raia na kupambana na wavamizi.

Shambulio la leo limetekelezwa miakamitatu baada yashambulio la al-Shabab katika kambi yao huko el-Adde nchini Somalia. Kundi hilo la Kiislamu liliteka na kudhibiti kambi ya majeshi ya majeshi ya Muungano wa Afrika mjini el-Adde na kuua wanajeshi 63 wa Kenya.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

 

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.