The House of Favourite Newspapers

Britam Tanzania Yatambulisha Bima Mpya za Matibabu – ‘Afya Care’ na ‘Amani Health’

0
Meneja wa Idara ya Bima za Afya wa Britam Tanzania, George Mwita akizungumza kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Britam Tanzania, Farai Dogo.

Dar es Salaam, Tanzania – Jumanne 06, Agosti – Katika kuunga mkono mkakati wa kusaidia kazi kubwa anayoifanya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma ya bima, Britam Insurance Tanzania imetambulisha bima zake mpya za matibabu ‘Afya Care’ na ‘Amani Health,’ mahususi kwa ajili ya kutoa huduma ya afya ya kina na unafuu kwa watu binafsi na familia.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Insurance Tanzania, Bw. Farai Dogo alisema, “Tunayo furaha kuitambulisha Afya Care na Amani Health, bidhaa ambazo zinaonyesha dhamira yetu ya kutoa huduma bora za bima ya afya kwa wateja wetu. Lengo letu ni kuleta utulivu wa akili kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya, na hivyo kuimarisha ustawi wa wateja wetu.”

Hivi ndivyo uzinduzi huo ulivyofanyika.

Amani Health ni bima ya afya mahususi kwa wafanyabiashara, makampuni na vikundi vilivyosajiliwa rasmi. Bima hii inatosheleza angalau wafanyikazi au vikundi kuanzia vitano (5) pamoja na wategemezi wao.

Kwa upande wake, Bw. George Mwita, Meneja wa Idara ya Bima ya Afya-Britam Insurance Tanzania aliongeza, ” ‘Afya Care’ ni bima ya afya ya kipekee kwa ustawi wa mtu binafsi na familia. Kama wewe unatafuta bima thabiti kwa ajili yako binafsi au familia, bidhaa yetu imuendwa kuhakikisha unapokea huduma bora za afya kwa bei nafuu.  Bima ya afya ya ‘Amani Health’, imeandaliwa kama mkakati mpana zaidi wa kusaidia ukuaji na maendeleo ya wafanyabiashara mbalimbali nchini Tanzania.”

Kwa kuongezea, bima hizi za afya (Amani na Afya Care) ni mkakati wa kusaidia kazi kubwa anayoifanya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma ya bima.

Bima zote mbili ‘Afya Care’ na ‘Amani Health’ zinatoa huduma ya wagonjwa wa kulazwa (Inpatient) na wagonjwa wasio wa kulazwa (Outpatient) kupitia mtandao wetu wa watoa huduma za matibabu kwa watu binafsi, vikundi na familia. Faida zimeundwa maalum kwa machaguo mbalimbali na kutoa viwango tofauti vya faida. Chaguo hizi zinatokana na viwango vitatu – POA, IMARA, na SUPER – kwa bei ya chini kama TZS 370,000. Faida za ziada zinazopatikana ni pamoja na Meno, Uzazi, Macho, Mkono wa Pole, na Urejeshaji wa Marehemu.

Huduma za nje ya nchi hutolewa katika nchi zote ambako Bima ya Britam inafanya kazi – Kenya, Uganda, Rwanda, Msumbiji na Sudan Kusini. Huduma za kimataifa na za rufaa zinatolewa ndani ya Afrika Mashariki na India.

Leave A Reply