The House of Favourite Newspapers

BROKEN ENGLISH YA SHILOLE KWA RAIS JPM NI ADHABU?

Zuwena Mohammed ‘Shilole’

JUZIKATI niliona video ya msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ akimkaribisha Rais John Pombe Magufuli katika mgahawa wake uitwao Shishi Food.

 

Katika video hiyo sikuona jambo baya kwani alichokuwa anakifanya ni kuitangaza biashara yake. Shida kubwa niliyoibaini ni kile Kingereza chake kibovu au wazungu wanakiita broken English aliyokuwa akiongea. Tatizo halikuwa yeye kuongea broken English kwa sababu kila mmoja anajua kuwa, katika kujifunza kitu lazima uanze kwa kukosea kidogo.

 

Shida niliyokuwa naiona ilikuwa ni ile kutumia nguvu kubwa sana kutamka maneno ya Kingereza na hata pale anapokutana na ugumu wa kuunda sentensi ya kueleweka, alikuwa akilia kwa uchungu huku akitoa maneno ya simanzi kuwa, anajua wapo watakaokuwa wanamcheka kwa ‘yai lake bovu’ lakini ipo siku ataongea vizuri hadi watashangaa.

 

Ukijaribu kuangalia ‘comments’ za watu mbalimbali walioingalia ile video, wapo waliosema kuwa ile ni staili yake ya kutafutia kiki na si kwamba machozi aliyokuwa akiyatoa yalikuwa ya dhati.

 

Kwangu mimi wakati anaanza kuongea, nilimchukulia tu kama mtu mwenye nia ya dhati ya kujifunza kitu na kwamba yupo tayari ku-share na mashabiki wake kila hatua anayopitia kuelekea kuongea Kingereza kizuri ila sasa kilio alichokuwa akikitoa na jinsi alivyokuwa akijishika kichwa, mara kifua katika kutengeneza sentensi za kueleweka ndivyo vilivyonishangaza.

Nikajiuliza kwamba, au atakuwa amepewa adhabu ya kuongea kizungu kila anapohojiwa? Kama ni hivyo, ni nani aliyempa adhabu hiyo na kwa sababu gani?

Nikaona ni jambo lisilowezekana, nikawa najiuliza tena kwamba, kulikuwa na sababu gani sasa za kulia kisa kuna watu wanamcheka kwa kuongea Kingereza kibovu? Na kama alikuwa anajiona kabisa hawezi kutengeneza sentensi nzuri, zilizonyooka za kumkaribisha rais kwenye mgahawa wake, kwa nini asingetumia tu Kiswahili? Yaani ni kama alikuwa anashurutishwa kwamba asipoongea Kingereza anauawa.

 

Hakika maswali yaliyonijia akilini kwangu yalikuwa mengi lakini mwisho nikaona kwamba, anachokifanya Shilole ni kujichoresha, labda iwe anafanya komedi. Lakini kama kweli video ile imejaa uhalisia, basi kuna shida na ni bora akajitathimini.

 

Nikaona ni jambo lisilowezekana, nikawa najiuliza tena kwamba, kulikuwa na sababu gani sasa za kulia kisa kuna watu wanamcheka kwa kuongea Kingereza…

MAKALA: Mwandishi Wetu

Comments are closed.