The House of Favourite Newspapers

Buchosa Wapokea Tsh Bil 2 Kutengeneza Barabara Vijijini

0

MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo amesmema Serikali kupitia wakala wa barabara vijiji (TARURA) umepeleka kiasi cha Sh 2bilioni kwa ajili ya kufungua mtandao wa barabara vijijini kwenye Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema.

 

Shigongo amesema hayo kwenye mikutano ya hadhara iliofanyika katika vijiji vya Kakobe, Irenza na Nyangaramila kata ya Irenza, Kazunzu na Nyangaramila katika jimboa la Buchosa. Amesema ndani ya miezi minne tayari wamekwisha pokea kiasi hicho cha fedha na ujenzi wa barabara moja hadi nyingine umeanza.

 

Amewatoa hofu wakazi wa jimbo la Buchosa wanaotumia barabara ya Luchili, Nyanzenda hadi Katoma ambayo imetengewa Sh 460 millioni itaanza kutengezwa baada wiki mbili zijazo na kumaliza kabisa tatizo la barabara hiyo katika maeneo hayo.

Kwa upande wao madiwani wa kata hizo wamesema matengezo ya barabara hizo yakikamilika thamani ya mazao ya wakulima yatapanda ukilinganisha na sasa ambapo wanashindwa kupeleka mazoa yao sokoni kutokana na ubovu wa barabara.

 

Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Nyanzenda, Samson Juma amesema kilio cha wakazi wa jimbo la Buchosa ni kupata barabara nzuri, maji, huduma za afya pamoja na elimu bora ambayo ndiyo mahitaji yao makuu.

 

Juma amesema mbunge Shigongo amepigania kupata fedha hizo zije kwa Wananchi ili ziwasaidie amefanya Jambo la heri ambalo wanabuchosa ndiyo kilio chao.

 

Wananchi wa jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wamemwombo mbunge wao kuhakisha barabara za Jimbo hilo zinatengenzwa na kupitika wakati wowote ili kukuza uchumi wa wananchi wa Buchosa.

Leave A Reply