The House of Favourite Newspapers

Bugatti la Ronaldo Lapata Ajali, Aaagiza Ndinga Mpya na Kuendelea Kula Bata

0
Gari la Ronaldo lilivyopata ajali

GARI la Kifahari la Supastaa wa Manchester United na Nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo limepata ajali baada ya kugonga nyumba kisiwani Mallorca, katika eneo la Sa Coma nchini Hispania.

 

Gari hilo aina ya Bugatti Veyron lenye thamani ya Pauni milioni 1.7 ambayo ni sawa na zaidi ya Bilioni 4.8 za kitanzania lilikuwa likiendeshwa na mfanyakazi wake, nyota huyo na familia yake hawakuwemo kwenye gari.

Nyota wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo

Dereva wa gari ameripotiwa kutoka bila majeraha lakini gari hilo limeharibika sana kwa mbele pia limeharibu vibaya sehemu ya mbele ya nyumba iliyoigonga.

 

Ronaldo pamoja na familia yake wamekuwa kisiwani humo tangu wiki iliyopita Juni 14, 2022 kwa mapumziko ambapo wamekodi nyumba ya kifahari katika eneo la Tramuntana Mountains kwa ajili ya kula bata.

 

Gari hilo ni moja kati ya magari mawili ambayo Ronaldo aliyasafirisha kwenda Mallorca kwa matumizi kipindi cha mapumziko.

 

Polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na tayari Ronaldo amesafirisha gari lake jingine aina ya Mercedes-Benz G-Class kuendelea kula bata.

Leave A Reply