The House of Favourite Newspapers

Buku ya Sokabet Yampa Denti wa Mzumbe Milioni 1

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichopo mkoani Morogoro, Mlack Ibrahim.

 

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichopo mkoani Morogoro, Mlack Ibrahim amefanikiwa kushinda shilingi milioni moja baada ya kubashiri katika kipengele cha Jackpot katika Kampuni ya Sokabet.

 

Ibrahim ambaye ni mwenyeji wa Dar amezungumza na gazeti hili na kusema kuwa kiasi hicho cha fedha amekipata katika muda sahihi kwa kuwa kimekuwa na msaada mkubwa katika masomo yake anayoendelea nayo.

 

Akifafanua ilivyokuwa mshindi huyo ambaye ana umri wa miaka 22 amesema alishiriki kipengele hicho wikiendi iliyopita ambapo mshindi anaweza kupata hadi zaidi ya shilingi milioni 100 ikiwa atapatia matokeo ya michezo 13.

 

“Unajua Jackpot ya Sokabet unatakiwa kupatia michezo 13 lakini kunakuwa na mitatu mingine ya dharura, sasa mimi nilipatia michezo kumi kati ya ile 13 ambayo nilitakiwa kupatia ndiyo nikashinda kiasi hicho cha fedha.

 

“Nimekuwa na kawaida ya kushiriki mara kwa mara na kupata fedha ndogondogo mara kwa mara lakini hii ni mara yangu ya kwanza kucheza na kupata kiasi kikubwa cha fedha, nililipwa muda mfupi tu baada ya kujulishwa kuwa nimeshinda,” alisema Ibrahim.

 

Kuhusu alivyoanza kushiriki katika mchezo huo anasema: “Nilianza kuingia baada ya kutumiwa SMS kutoka kwao wenyewe Sokabet, nilikuwa sijui wanabashiri vipi kwenye tovuti yao, nilipotumiwa hiyo SMS nikabonyeza ‘link’ yao na kuendeleaa kufuatili na kujifunza huko baada ya kuingia ndani.

 

“Kabla ya hapo niliwahi kubeti katika zile huduma za makaratasi lakini nilivyoingia kwenye Sokabet nimeona mambo ni rahisi na unabeti mtandaoni bila kusumbuka na makaratani, ukipatia unalipwa fedha zako wala siyo watu wa longolongo kwa kuwa kuna siku nilikwama nikazungumza na watoa huduma wao wakanipa maelekezo vizuri.”

 

Akizungumzia jinsi wenzake walivyopokea ushindi wake alisema: “Kwa ufupi ni kama nimekuwa balozi mzuri, wengi walikuwa hawaamini kama mtu unaweza kushinda, tena nimeshinda kwa kubeti kwa shilingi 1000 tu, nilipotumiwa SMS kuwa nimeshinda na baadaye fedha kuingia kwenye akaunti yangu ya Sokabet ambayo wao wanakuingizia huko kisha unatoa kuingiza kwenye simu.

 

“Nilikuwa na furaha sana na nimewashawishi wengi kujiunga pia kwenye huduma zao Sokabet hasa wanafuzni wenzangu wa Mzumbe.”

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Comments are closed.