BULAYA Acharuka Kikokotoo Kipya cha Mafao, Awavaa CCM – Video

Mbunge wa Jimbo la Bunda, Ester Bulaya, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ametoa shutuma kwa watendaji wakuu wa SSRA akidai kuwa ni waongo wanapotosha umma juu ya ubora wa kikokotoo kipya cha mafao ya wastaafu, wakidai ni bora Afrika Mashariki huku akitolea mfano wa vikokotoo vya nchi za Kenya na Uganda.

 

Bulaya amesema hayo leo Desemba 4, 2018 wakati akizungumza na Wanahabari kuhusu kikokotoo hicho na kusema kupongezwa na Spika Job Ndugai kuhusu asilimia 25% ya mafao ya wastaafu hakuondoi ukweli kuwa chanzo ni wabunge wa CCM kutumia wingi wao na kutoheshimu mawazo ya mbadala ya kambi ya upinzani.

 

“Tunamtaka Waziri husika (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Walemavu) atoke na aseme ni kwanini mchakato huu wa kubadili kikokotoo haukupita kwenye vikao halali kabla ya kufika hapo. Mimi kama Waziri Kivuli wa Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Walemavu na jopo langu, tutahakikisha tunaandaa muswada binafsi na kuupeleka Bunge kama tu kikokotoo hiki hakitarekebishwa,” amesema Bulaya.

VIDEO: TAZAMA VIDEO AKIFUNGUKA

Toa comment