The House of Favourite Newspapers

Bulaya Augua, Kesi ya Kina Mbowe Yakwama – Pichaz

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuanza kusikiliza utetezi wa viongozi tisa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) akiwemo mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, baada ya  mshtakiwa Ester Bulaya kudaiwa kuwa mgonjwa.
Wakili wa utetezi Prof. Abdallah Safari  ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba, kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kuanza utetezi lakini mdhamini wa Bulaya amewapa taarifa kuwa anaumwa na amelazwa hospitali.
Prof. Safari aliiarifu mahakama kuwa kwa mujibu wa sheria, kwa sababu mshtakiwa Bulaya hayupo hawawezi kuendelea na utetezi hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Thomas Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 15, 17 na 18 mwaka huu ambapo washtakiwa hao wataanza kujitetea.
Washtakiwa hao wanaanza kutoa utetezi wao baada ya mashahidi  wanane wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao na mahakama kuwaona washtakiwa hao wana kesi ya kujibu.
Wanaokabiliwa katika kesi hiyo  ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu;  Naibu katibu Mkuu Bara;   Mbunge wa Kibamba, John Mnyika;  Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche; Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, na  mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.
Wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko;  na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.
Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendajia jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, jijini Dar es Salaam.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Comments are closed.