The House of Favourite Newspapers

Bunge Latengua Kanuni Kujadili Mpango wa Serikali

0

bu4Akitengua kanuni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu katika Serikali ya Awamu ya Tano, Jenista Mhagama amesema kwamba bunge lilitakiwa likae kama kamati mwezi Nombemba ili liweze kujadili mpango wa serikali lakini kutokana na uchaguzi mkuu uliokuwepo nchini kazi hiyo ilishindikana.

Kwa msingi huo kutokana na uwezo wa bunge kupitia ibara ya 63 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayowezesha bunge kujadili mipango ya serikali,kwa muda muafaka serikali imeamua kutengua kanuni ili bunge likae kama kamati kwa muda wa siku 5 ili kujadili mpango wa serikali ili wabunge waweze kuishauri serikali kabla ya bunge la bajeti.

Aidha mpango huo ulishindwa kujadiliwa bungeni hapo juzi kutokana na kanuni za bunge kukiukwa kwa kusomwa bila kutengua kanuni ya 94(1).

Leave A Reply