The House of Favourite Newspapers
gunners X

Bunge SC Watamba Kunyakua Ubingwa wa Afrika Mashariki

0
Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, William Ngeleja akifunguka walivyojipanga.

UONGOZI wa Timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bunge Sports Club umetamba kuwa umejiandaa vyema kunyakua Ubingwa wa Mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki (Inter Parliamentary Games) yatakayoanza kutimua vumbi Disemba Mosi, mwaka huu jijini Dar kwenye Viwanja vya Taifa na Uhuru.

Wachezaji wa Bunge Sports Club wakifuatilia mkutano huo.

Mashindano hayo yatakayashiorikisha Mabunge ya Nchi za Afrika Mashariki zikiwemo Uganda, Kenya, Sudan Kusini, Rwanda, Burundi na wenyeji Tanzania, huku michezo saba ya soka, gofu, riadha, kuvuta kamba, pete na kutembea kwa mwendokasi ndiyo itashindaniwa.

Mkutano ukiendelea.

Akizungumzia juu ya maandalizi yao, Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, William Ngeleja amesema kuwa lengo la timu yao ni kuchukua ubingwa wa mashindano hayo ambapo kwa sasa wanaendelea na mazoezi ili kufanikisha suala hilo.

“Tumejiandaa kuhakikisha kwamba tunachukua ubingwa wa Mashindano ya Mabunge, na sasa tunaendelea na mazoezi yetu lakini kwa ajili ya kujiweka sawa,” alisema Ngeleja.

Musa Mateja | GPL.

Matukio kama haya na mengine, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply