The House of Favourite Newspapers

Bunge Tanzania Haikamatiki, Uganda Wasusa

Mchuano ukiendelea kati ya Tanzania na Uganda.

 

TIMU ya Mpira wa Pete (Netiboli) ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana Desemba 6, 2017, asubuhi iliibuka na ushindi wa mabao 13-11 dhidi ya wapinzani wao Uganda katika michuano ya Timu za Mabunge ya Afrika Mashariki inayoendelea katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Tanzania 13 – 11 Uganda.

Katika mechi hiyo, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Ndani, kila timu ilionyesha ushindani mkubwa kutokana na kuhitaji ushindi licha ya mechi hiyo, kuingia doa kidogo baada ya wachezaji wa Bunge wa Uganda kumvamia mwamuzi kwa kile walichodai kuonewa na maamuzi yaliyokuwa yakitolewa.

 

Tanzania wakishangilia.

Wakati wachezaji wakimvamia mwamuzi huyo, Jeshi la Polisi liliingilia kati kwa ajili ya kumuokoa na kuwekwa chini ya uangalizi mkubwa ambapo mechi hiyo ilisimama kwa dakika 20 huku malumbano makubwa yakitawala uwanjani hapo kabla ya mwamuzi huyo kumaliza mechi hiyo kwa Tanzania kushinda mabao 13-11.

NA MUSA MATEJA  | GPL

SHUHUDIA VIDEO DK SHIKA NA EBITOKE WAKIFUNGUKA

Comments are closed.