The House of Favourite Newspapers

Bungeni: Mtolea Amtaka Rais Asihudhurie Sherehe za Mapinduzi – Video

 

MBUNGE wa Jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea amesema ni bora Rais wa Jamhuri ya Muungano asihudhurie Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar akidai kuwa siyo utaratibu mzuri kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kutangulia kuingia kwenye viwanja vya sherehe hizo kisha kusimama na kumpokea Rais wa Zanzibar.

 

Mtolea amesema hayo bungeni Mjini Dodoma leo, na kuongeza kwamba ingekuwa busara zaidi kama Rais Magufuli asingehudhuria kwenye sherehe hizo badala yake angeweza kumtuma hata Naibu Waziri wa Mazingira na akaiwasilisha serikali.

 

Mbunge huyo alienda mbele zaidi na kudai kwamba wabunge wa Zanzibar wamekuwa na chombo chao cha kueleza kero zao kuhusu Masuala hayo ya muungano, pia wamekuwa wakiungana bila kujali itikadi za vyama zao kuzungumzia masuala ya Zanzibar kwenye Muungano jambo ambalo amedai, Tanzania Bara hakuna chombo hicho.

 

Aidha, Mtolea amesema ili Muungano uweze kuimarika na kuuboresha, ni vyema hoja za Muungano zikasikilizwa na kutatuliwa badala ya kuzuia mijadala ya hiyo.

 

VIDEO: MSIKIE MTOLEA AKIFUNGUKA

Comments are closed.