The House of Favourite Newspapers
gunners X

Bupandwa FC Yaibuka Mabingwa wa Bonanza la Shigongo kwa Penati 3–0

0

Timu ya Bupandwa FC imeibuka mshindi wa Bonanza la Shigongo la Kufunga Mwaka, baada ya kuichabanga Katwe FC kwa mikwaju ya penati 3–0, kufuatia sare ndani ya dakika za kawaida.

Bonanza hilo limefadhiliwa na Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, likiwa na lengo la kuburudisha wananchi pamoja na kuimarisha mshikamano na ushirikiano wakati wa kuukaribisha mwaka mpya 2026.

Katika bonanza hilo, Bupandwa FC imepokea zawadi ya Shilingi 300,000, huku Katwe FC wakiondoka na Shilingi 200,000 kama mshindi wa pili.

Akizungumza baada ya fainali hiyo, Shigongo amewataka wananchi wa Buchosa kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na amani, akisisitiza kuwa michezo ni chombo muhimu cha kuwaleta watu pamoja na kuimarisha maendeleo ya jamii.

Leave A Reply