The House of Favourite Newspapers

#GlobalCelebrities: Burna Boy Ala POVU La Wakenya Baada Ya Kushindwa Kufanya Show Yenye Kiwango – (Twitter)

Ukitaka kuona umoja wa Wakenya fanja jambo uzingue alafu lipeleke kwenye mitandao ya kijamii, hawatokuacha bure! 

Msanii wa Nigeria Burna Boy hivi karibuni amejikuta akila POVU la Wakenya kwenye Twitter baada ya kushindwa kufanya preformance yenye kiwango kwenye moja ya clubs jijini Nairobi… Ilikuaje? Ipokee hii.

Kwa mujibu wa baadhi ya mitandao ya Kenya, Burna Boy aliingia makubaliano ya kufanya show na Club Westlands jijini Nairobi lakini licha ya kufika kama ilivyoahidiwa msanii huyo alichelewa kupita kiasi na kushindwa kutoa show yenye kiwango cha thamani ya pesa ilyolipwa na wahudhuriaji usiku huo wa Mosi 1 April 2017. Wengine wameendelea kuripoti kuwa Burna Boy alifanya show ya lisaa lizima lakini kwa kulipuwa na muda wote aliyokuwa stejini msanii huyo alionekana amelewa.

Bila kumvutia pumzi, Wakenya wenye uchungu na pesa yao wakamwendea Burna Boy mtandaoni wakimtaka awarudishie pesa ya viingilio ikiwa kama fidia halali kwa kutoa show mbovu iliyokuwa chini ya kiwango. Kwa upande wake Burna Boy hakupendezhwa na jambo hilo hivyo kuanza kuwajibu na kuwatukana baadhi ya mashabiki hao na hata kuwablock baadhi yao.

Kilichofuata baada ya hapo ni mapovu ya Wakenya kwa Burna Boy.

Hizi ni baadhi ya Tweets nilizofanikiwa kuzipata zikitumia hashtag ya #BurnaBoyBlockChallenge:

ReTweet kama ulikuwa hujui kuwa Burna Boy alikuwa Kenya..

Burna Boy atoa mkwara kama wa Davido. Wanigeria wote matapeli lakini. Muulize mtu yoyote kutoka Donholm.”

Chris Brown ni supastaa alikuja Kenya kwa wakati kutoka USA lakini Burna Boy ambaye ni Muafrika anakuja saa kumi asubuhi alafu #KOT (Kenyans On Twitter) watulie?

Hatimaye! Burna Boy Mnigeria mjinga kuliko wote kaniblock. Nilaanza kuwaza pengine mimi sio Mkenya #BurnaBoyBlockChallenge.” 

#BurnaBoyBlockChallenge mtoto anayejiita Bunsen Burner kawablock wanaume kwenye Twitter, hamuwezi mkaamini.

Oya Donald Trump huyu Burna Boy ana Blocks nyingi, anaweza kukusaidia kujenga ule ukuta wa Mexico #BurnaBoyBlockChallenge.

Burna Boy ni pepo la ki-IGBO… Sikijua kama hana jina maana hata sikujua kama yupo Kenya…” 

#BurnaBoyBlockChallenge Huyu mjinga Burna Boy hajui kuwa#KOT (Kenyans On Twitter) ni Serikali ya 4 Kenya. Kutublock ni sawasawa na kumchokoza nyoka…” 

Niambie, huyu ndio angekuwa amekuja Tanzania na amefanya hivi,  unadhani watu wangemshambulia wapi zaidi, Twitter ama Instagram? Niachie comment yako hapo chini.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

 

Comments are closed.