Burna Boy, Tiwa Savage Kutokanyaga Sauzi

Image result for burna boy

MWANAMUZIKI wa miondoko ya Afrobeat nchini Nigeria, Damini Ogulu maarufu kama Burna Boy, ameapa kutokanyaga ardhi ya Afrika Kusini baada ya kutokea ghasia dhidi ya raia wa kigeni.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Burna Boy ame-tweet akisema hajawahi kukanyaga nchini Afrika Kusini tangu mwaka 2017 lakini hawezi kwenda tena hadi serikali ya Afrika Kusini itakaposhughulikia suala hilo.

 

Burna Boy aliendelea kutweet akisema: ”Naelewa mateso waliyopitia miaka mingi iliyopita imewafanya wa-Afrika Kusini kuchanganyikiwa kiasi cha kuwachukulia kama maadui watu waliowasaidia wakati wa utawala wa kibaguzi.”

Aliongeza kuna raia wa Afrika Kusini ni ”watu wazuri na wapenda maendeleo… lakini kwa hili wamekosea”.

Mwanamuziki Tiwa Savage naye hakukaa kimya, ameamua kufutilia mbali shoo ya tamasha la DSTV Delicious Festival litakalofanyika jijini Johannesburg Septemb 21 mwaka huu baada ya kuchukizwa na matukio yanayoendelea nchini Afrika Kusini.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Tiwa Savage ame-tweet kuwa hawezi kuvumilia vitendo vya kikatili vinavyofanywa  dhidi ya Wanigeria wenzake nchini Afrika Kusini.

” width=”20″ height=”20″>


Loading...

Toa comment