The House of Favourite Newspapers

Busu la Wema Lamdatisha JB

0

jb na wema (2)Waigizaji nguli wa sinema za Kibongo, Jacob Stephen na mwenzake Wema Sepetu ‘Madam’.

Mwandishi wetu

MKONGWE kwenye anga la sinema za Kibongo, Jacob Stephen ameeleza jinsi alivyodatishwa na busu la mwigizaji mwenzake Wema Sepetu ‘Madam’ wakati wakirekodi sinema yake mpya iitwayo Chungu cha Tatu.

jb na wema (1)JB alisema licha ya kuwa busu hilo lilikuwa katika moja ya scene ya filamu hiyo iliyoingia sokoni Jumatatu iliyopita, lakini lilimfanya akose amani kutokana na Wema alivyolipiga kwa mbwembwe na kuonesha hisia zilizopitiliza utafikiri ni la kweli.

“Mh! Alinifanya nipagawe kidogo lakini ndiyo kazi. Unajua lazima mtu aoneshe uhalisia katika filamu ili iweze kumgusa pia mtazamaji, kwa ujumla sinema ni kali na namshukuru Mungu imekuwa gumzo kila kona, naomba mashabiki waendelee kuniunga mkono,” alisema JB.

Leave A Reply