The House of Favourite Newspapers

Busungu aweka rekodi ya kipekee Yanga SC

0

IMG_201506175_121423

Malimi Busungu.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam
AKIMCHEZESHA nafasi tano ndani ya uwanja, Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ametamka kuwa anajivunia kuwa na mchezaji aina ya Malimi Busungu ambaye anaonyesha kiwango kikubwa.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Toto kwenye Uwanja wa Taifa juzi jijini ambapo Yanga ilishinda mabao 4-1.

Busungu aliyetua kuichezea timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mgambo, ameshapangwa katika nafasi tano tofauti uwanjani, jambo ambalo ni la kipekee.

Amewahi kupangwa namba 7, 9, 10, 11 na 2 zote akionyesha kuzimudu na kufanya vizuri, ambapo beki wa kulia alipangwa baada ya Juma Abdul kupata majeraha na kutolewa katika mchezo wa juzi.

“Busungu ni mchezaji wa kipekee, kila ninapompanga anaweza, safi sana. Kasi yake imemsaidia sana katika kupandisha mashambulizi na kurudi kukaba, pia ametengeneza nafasi ya bao, ni kitu kizuri,” alisema Pluijm.

Leave A Reply