The House of Favourite Newspapers

Busungu: Pluijm alinipa jukumu la  kumtoa mchezoni Tshabalala

0

IMG_0371

Malimi Busungu.

Nicodemus Jonas Dar es Salaam

STAIKA aliyewalaza mapema Simba juzi Jumamosi, Malimi Busungu, ametoboa siri ya benchi la ufundi na kutaja sababu ya kuingizwa dakika za mwanzo kabisa kuchukua nafasi ya Simon Msuva aliyeonekana kuchemka kwenye mechi hiyo.

Katika mchezo huo ambao Simba walilala mabao 2-0, Busungu aliyefunga bao la pili baada ya lile la awali la Amissi Tambwe, alisema kocha wake, Hans van Der Pluijm, alimpa jukumu moja tu; kuhakikisha Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ haendelei kuwasumbua.

Simba ilianza mpira kwa kasi ya ajabu huku mabeki wake wa pembeni, Tshabalala na Hassan Kessy, wakionekana tishio kwa kuwanyanyasa mawinga wa Yanga, ndipo Pluijm alipomtoa Msuva na kumuingiza Busungu dakika ya 35 ambapo kuanzia hapo kasi ya Simba ilipungua kwa asilimia kubwa.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Busungu alisema: “Kikubwa kocha aliniambia kitu cha kufanya ni kuhakikisha nampa kashikashi Tshabalala, maana alionekana kusumbua sana, alikuwa huru sana, ndicho alichonisisitizia sana. Na kweli namshukuru Mungu nilifanikiwa kutimiza kile alichotaka kocha.”

Leave A Reply