Bwalya: Tunazidi Kuingia Kwenye Mfumo wa Kocha

RALLY Bwalya, kiungo wa Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco amesema kuwa bado wanaendelea kuingia kwenye mfumo wa kocha huyo ambaye anawasisitizia wapambane kupata matokeo.

Pablo alibeba mikoba ya Didier Gomes ambaye alibwaga manyanga kutokana na timu hiyo kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sasa ana kazi ya kupambania Kombe la Mapinduzi lililo mikononi mwa Yanga.

Bwalya mkononi ana tuzo ya mchezaji bora wa mchezo ambayo aliipata kwenye mchezo dhidi ya Selem View uliochezwa Uwanja wa Amaan wakati Simba ikishinda kwa mabao 2-0.

Nyota huyo alisema: “Kikubwa ambacho tunakifanya ni kuona kwamba tunapata matokeo na tunazidi kuona namna gani tunaweza kwenda na mfumo wa mwalimu ambaye anatufundisha na amekuwa akituambia kwamba tunapaswa kushinda mechi zetu ambazo tunacheza.”

Simba imetinga hatua fainali ya Kombe la Mapinduzi jana baada ya kuitungua Namungo FC kwa bao 2-0. Simba atakutana fainali ya AZAM FC ambaye alimfunga Yanga katika nusu fainali ya kwanza kwa mikwaju ya penati 9-8 baada ya kutoka sare dakika 90.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment