The House of Favourite Newspapers

Bwalya: Tutaamka na Kufanya Vyema

0

KIUNGO wa Simba Larry Bwalya, amefunguka mipango yake msimu huu kwenye Ligi Kuu na Ligi ya Mabigwa, huku akisema watafanya vizuri.

Mzambia huyu huu ni msimu wake wa pili akiwa na Simba na sasa anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji watakaowika zaidi msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mzambia huyo amesema kuwa anaamini atakuwa na msimu bora sana.

“Nimejipanga vizuri kuisaidia timu yangu kwenye Ligi ya Mabingwa na hata Ligi Kuu Bara naamini kuwa kazi hiyo naiweza

“Ligi ni ngumu ila tushaizoea tutapambana kutetea nafasi yetu kwa kuwa uwezo huo tunao,” alisema Bwalya.

REEN OSCAR, Dar es Salaam

Leave A Reply